Gachagua UDA

Naibu wa rais Rigathi Gachagua ameeleza kwamba Serikali ya Kenya kwanza haitaruhusu kwa vyovyote vila kuwapa viongozi wa upinzani nafasi katika serikali.

Akizungumza kwenye kongamano lililowaleta pamoja wajumbe wa chama cha UDA jijini Nairobi, Gachagua amesema kuwa uongozi uliopita ulitekeleza wajibu wake isivyofaa kwa kukubali upinzani kupenyeza katika serikali, jambo alilosema halitakubalika kivyovyote kwenye uongozi wa rais William Ruto.

Gachagua pia ameahidi kusaidia kuimarisha chama cha UDA, kwa huhakikisha kwamba chama hicho kinapata angalau Ofisi moja katika kila kaunti, ili kuendelea kujiimarisha kuelekea kwa chaguzi za usoni.

 

May 18, 2023