Aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta amewashutumu baadhi ya viongozi kwa kuwatusi wengine wakati wa ibada za Kanisa.

Akizungumza Jumatatu wakati wa Kongamano la Kitaifa la Wajumbe wa Jubilee jijini Nairobi, Uhuru alisema alama ya njiwa ya Jubilee inawakilisha amani.

Katika shambulio linaloonekana dhidi ya Rais William Ruto na washirika wake, Uhuru aliwakashifu viongozi wa Kenya Kwanza kwa kurushiana matusi kwenye sherehe za kanisa.

Uhuru alisema nia ya chama cha Jubilee ni kuleta amani nchini.Aidha kiongozi huyo wa zamani aliwaambia wajumbe wa chama cha Jubilee kuwa ataendelea kuwahudumia hadi watakapomtaka aondoke madarakani.

May 22, 2023