Mama mjamzito alijifungua nyumbani kwa msaada wa wakunga ambao mara kwa mara walikua kina Nyanya.
Katika miaka ya kale, mfumo wa elimu unaotambuliwa na kuzingatiwa kwa sasa haukuwako, hivyo basi watoto walipata mafunzo yao moja kwa moja kutoka kwa wanajamii wengine, kwa kuzingatia jinsia zao. Watoto wa kiume walitangamana sana na wazee na hasa babu zao ili waweze kufahamu jinsi ya kuishi kama wanaume. Watoto wa kike nao walitangamana na nyanya, shangazi na kina mama wengine na kupokea mafunzo yao kuhusu jamii. Mafunzo pia yalitolewa kwa kusikiliza hadithi, vitendawili na mafumbo methali pamoja na kuimba nyimbo.
Iwapo una malalamishi yoyote kuhusiana na Makala haya Wasiliana nasi, au uwasiliane na John Waicua kwa barua pepe j.waicua@radioosotua.co.ke