Rais William Ruto hivi leo ameongoza mkutano kuhusu uwekezaji barani Afrika jijini Nairobi.

Rais Ruto akizungumza kwenye mkutano huo alipendekeza bara la Afrika kuimarisha mfumo wa biashara kwa kutumia sarafu zake ili kupunguza kutegemewa kwa utumizi wa dola.

Ameongeza kuwa hatua hii itafungua nafasi kubwa ya kibiashara kati ya mataifa ya Afrika. Kando na suala la sarafu, alieleza kuwa Afrika lazima itengeneze miundombinu yake ili kuchochea biashara ya kikanda.

Hali kadhalika alizirai serikali za Afrika kushirikiana na sekta za binafsi ili kuafikia malengo ya kuimarisha miundo mbinu.

May 29, 2023