Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki ametoa agizo la kutiwa nguvuni kwa viongozi wote waliohusika katika vurugu zilizoshuhudiwa katika mpaka wa maeneo ya Nkaararo na Enoreteet huko Trans Mara, Kaunti ya Narok.
Akizungumza Siku ya Jumatao ya leo katika kaunti ya Turkana alikoelekea katika zoezi la ukaguzi wa jinsi Operesheni ya maliza Uhalifu inaendelea, waziri kindiki alimwagiza mratibu wa seriklai katika ukanda wa bonde la ufa Dk. Hassan Abdi kuwakamata viongozi wote waliohusika na mapigano hayo mapya yaliyosabaisha nyumba na mashamba ya watu katika eneo hilo kuchomwa.
Tutashirikiana na viongozi wote na wananchi kwa jumla kuhakikisha matatizo ya usalama yanashughulikiwa kikamilifu.
— Kithure Kindiki (@KindikiKithure) June 7, 2023
Waziri Kindiki alieleza kwamba kiongozi yeyote aliyehusika na ghasia hizo atashtakiwa pasi na kuangazia misimamo yao ya kisiasa. Idadi isiyojulikana ya watu waliumia katika vurugu hizo siku ya jana baada ya kuteketezwa kwa nyumba zao huku mzozo ulioanza siku ya Jumapili ukiendelea kutokota.
Meeting Turkana County leadership, led by Governor Jeremiah Lormukai, for consultation and deliberations on security, development, and delivery of Government services. pic.twitter.com/8neH8BuL4b
— Kithure Kindiki (@KindikiKithure) June 7, 2023