BY ISAYA BURUGU 13TH JUNE,2023- Serikali imetangaza kuwa itaanza kuwazawadi wanariadha wanaovunja rekodi ya ulimwengu shiingi Milioni  tano.Akizungumza wakati wa mkutano na wanariadha katika ikulu ya Nairobi mapema leo,rais Wiliam Ruto pia amesema kuwa serikali itatembea na wanariadha na kuwaunga mkono kuelekea mbele na pia kuwatuza kwa kuinua hadhi ya taifa hili kimataifa.

Wakati wa mkutano huo rais ametangaza kuwa serikali itamzawadi Faith Kipyegon Shiingi milioni tano na nyumba ya dhamani ya shilingi milioni sita.

Hii ni baada ya Kipyegon kuvunja rekodi ya dunia kwa mbio za mita 5000 nchini Italia mwishoni mwa juma sawa  na nyingine ya mita 15000.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

June 13, 2023