Mawakili wawili, George Kariuki na Elisha Komora, waliokuwa wakiwakilisha mhubiri mwenye tata Paul Mackenzie na washtakiwa wenzake wamejiondoa katika kesi inayomkabili mhubiri huyo.

Wakizungumza na waandishi wa habari, wawili hao walisema kujitoa kwao kumetokana na hali ya kukatishwa tamaa na serikali katika kushughulikia kesi dhidi ya wateja wao.

Aidha wakili wa tatu, Wycliffe Makasembo, alisema ataendelea kuwawakilisha watuhumiwa hao huku akitoa wito kwa hakimu mkuu wa mahakama ya Shanzu Yusuf Shikanda kujiepusha na shinikizo zozote za nje zinazojaribu kudhibiti mkondo wa kesi hiyo.

Mapema hii leo mahakama hiyo ya Shanzu ilifahamishwa kwamba wafuasi 16 wa mhubiri huyo wamekuwa wakisusia kula na kunywa kwa siku saba sasa.

June 14, 2023