Tovuti ya KUCCPS imefunguliwa tena kwa awamu ya pili  ambapo wanafunzi waliotuma maombi ya kujiunga na vyuo mbalimbali watapata fursa ya kufanya masahihisho ya chaguo lao.

Zoezi hilo litawapa wahitimu wa shule za sekondari fursa nyingine ya kuomba kozi zinazotolewa katika vyuo vikuu na vyuo vya ufundi.

Zoezi hilo litaendelea hadi Juni 27, 2023.

KUCCPS pia imewataka watahiniwa waliopata gredi ya C+ na zaidi katika mtihani wa KCSE wa 2022 na hawakupata fursa ya masahihisho ya kwanza kuhakikisha kwamba wametuma maombi ya masomo ya digrii au TVET katika kipindi cha sasa.

June 16, 2023