Waziri wa usalama wa ndani prof. Kithure Kindiki amewaagiza maafisa wa utoaji wa vitambulizho kufanya kazi hiyo bila ubaguzi.

Akizungumza katika kaunti ya Lamu, Kindiki ameagiza vitambulisho hivyo kutolewa katika muda wa siku 21 ili kuwapa wakaazi wa kaunti hiyo uhuru wa kupokea huduma za serikali.

Aidha amezirai jamii zinazoishi Lamu kuishi kwa utangamano akidai kuwa kila mmoja ana haki ya kumiliki mali na kufanya kazi katika kaunti hiyo huku akiwaonya wanaochochea uhasama kuwa watachukuliwa hatua za kisheria.

June 16, 2023