BY ISAYA BURUGU 17TH JUNE,2023-Chama UDA kimetuma risala za rambirambi kwa jamii ndugu na marafiki   wa mwakilishi wadi wa Chewani  Hamisi Iddi Deye aliyefariki dunia leo asubuhi kufuatia ajali ya barabarani.

Kupitia taaifa chama hicho kimesema mwakilishi wadi huyo wa bunge la kaunti ya tana river  ameaga dunia kufuatia ajali iliyotokea katika barabara kuu ya Malindi -Garsen.

Hadi wakati akiaga dunia MCA huyo  amekuwa kiongozi wawachache katika bunge la kaunti ya Tana river.

Haikubainika haraka  kilichofanyika kabla ya ajali hiyo .

Kifo chake kinajiri siku kadhaa tu baada ya katibu mkuu wa chama hicho Cleophas Malala kuzindua kampeni ya kuwasajili wannachama zaidi wa UDA kote nchini.

 

 

 

June 17, 2023