BY BURUGU ISAYA  20TH JUNE,2023-Rais  William Ruto hivi leo amefungua rasmi warsha ya hadhi ya juu ya kawi YA MWAKA HUU barani Afrika inayoandaliwa katika jumba la mikutano la KICC.Warsha  hiyo itazamiwa kukamilika ijumaa wiki hii.

Rais akizungumza kwenye hafla hiyo amelezea haja ya mataiafa ya Afrika kuungana katika kufanisha juhudi zitakazopelekea bara hili kuwa na kawi safi na hivyo basi kufanikisha juhudi za utunzaji amzingira.

Rais ameongeza kuwa Kenya imo mbioni kutekeleza jukumu lake kuelekea katika kupata suluhu baada ya kuzindua kiwanda cha kutengenezaji mitungi ya gesi kwa lengo la kupunguza kabisa bei ya mitungi yenyewe.

Kwa upande wake Waziri wa kawi Davis Chirchir amedokeza kuwa  warsha hiyo itatoa fursa mwafaka kama jukwa la kufanikisha ushirikiano ,kutambua fursa  na kusongesha sekta hiyo mbele.

 

 

June 20, 2023