BY ISAYA BURUGU,21ST JUNE,2023-Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Olentutu amewahimiza wananchi wa kaunti hii kutunza mazingira.
Akizungumza katika hoteli moja katika kaunti hii, amesema kuwa msitu wa Mau ,Loita na nyakware iko katika hatari ya kuangamia kutokana na shughuli za kibindamu haswa ukataji miti.
Hata hivyo amesema kuwa maafisa wa polisi wakishirikiana na machifu pamoja na wazee wa kijiji, wako tayari kuwakamata wauzaji wa makaa na kuongeza kuwa kuna pia wale wanao chimba mchanga karibu na barabara nao pia watachukuliwa hatua kali.
Audio Player