BY ISAYA BURUGU 24TH JUNE 2023-Mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha ODM John MBadi anawataka wabunge walioenda kinyume na msimamo wa chama cha ODM na kupigia kura mswada wa kifedha wa mwaka 2023 wajiuzulu nyadhifa zao na kutafuta upya nafasi za uwakilishi kutoka kwa wananchi.

Mbadi anasema iwapo wabunge wa ODM wanahisi kuwa hawawezi  kuunga mkono msimamo wa chama chao na sera hawana budi kujiuzulu na kusaka nafasi zao kutumia chama kingine.Amewataja mbunge wa Gem Melesho Odhiambo na mwanzake wa Bondo Gideon Ochanda akiwataja kama miongoni mwa wabunge waasi akisema kuwa kama chama watachukua hatua zifaazo.

Mwenyekiti huyo wa ODM aliyasema hayo alipohudhuria mkutano wa kiasiasa katika eneo bunge la Gem akiwa ameandamana na wabunge kadhaa akiwemo mbunge wa Ugunja Opiyo WANDAYI  na seneta wa Kitui Enock Wambua miongoni mwa viongozi wengine.

Gavana wa Siaya James Orengo anasema kuwa wanafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa taifa linasimamiwa vyema.

 

June 24, 2023