Maaskofu wa kanisa katoliki wanaoongoza maeneo ambayo hushudia mizozo mara kwa mara, hii leo wamezindua kampeni ya amani mjini Eldoret.

Kampeni hiyo inapaniwa kupiga jeki juhudi za serikali kumaliza uhasama katika maeneo hayo ya kaskazini mwa bonde la ufa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, askofu wa jimbo katoliki la Ngong’ John Oballa Owaa ameeleza kuwa njia mojawapo ya kuleta amani katika maeneo hayo ni kuwaleta pamoja washikadau wote wanaohusika na masuala ya amani humu nchini ili kujadili na kuweka mikakati ya kudumu.

June 28, 2023