BY ISAYA BURUGU,28TH JUNE,2023-Baada ya takribani siku kumi na moja ya kutoweka kwa aliyekuwa  mfanyikazi wa hazina yakitaifa Tom Osinde ,afisa huyo amepatikana katika mto Kuja kaunti ya Migori akiwa amefariki.Mwili wake umepatikana mwendo wa saa tano  usiku wa leo na kupelekwa katika hifadhi ya maiti mjini Migori.

Tayari washukiwa wawili wa mauaji hayo wamekamatwa na polisi. Wawili  hao ni wafanyikazi wa marehemu.Mmoja  wawashukiwa alikuwa ameliendesha gari la marehemu na kuliegesha kule transmara  siku aliyotoweka marehemu.

Siku moja kabla ya gari la marehemu kupatikana,Mshukiwa aliyejulikana kama Julius Mgoi alikuwa ameliendesha gari la marehemu hadi nyumbani kwake kule Mugirango kusini huku akidai kuwa mwajiri wake alikuwa amemtuma kuwasilisha stakabadhi Fulani kabla ya gari lenyewe kuendeshwa hadi Transmara eneo la enosuyian ambapo liliachwa  huko.

Baadaye alikamatwa na kuwaelekeza polisi hadi mto Kuja ambapo alidai alitupa mwili wa marehemu

.Uchunguzi wa mauaji hayo sasa unaelekezwa nyumbani kwa marehemu kule Ngata kaunti ya Nakuru huku maafisa wa upelelezi wakilenga kutanzua sababu za kifo chake.

June 29, 2023