Afya

Muungano wa Maafisa wa kimatibabu nchini KUCO umetishia kukatiza huduma zao kuanzia tarehe kumi na nne mwezi ujao wa Julai, ili kulalamikia utepetevu serikali katika kushughulikia maslahi ya wahudumu wa Afya.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Bw. Peterson Wachira, viongozi wa muungano huo wamelalama kwamba serikali inazembea katika kuidhinisha mikataba ya maelewano iliyoafikiwa hapo awali, kwa madhumuni ya kuimarisha utendakazi wao.

Zaidi ya hilo pia viongozi hao wamependekeza kuhusishwa kwa wakenya kabla ya kuidhinishwa kwa mapendekezo ya kuongeza zaidi fedha wanazotozwa chini ya mpango wa NHIF.

June 29, 2023