Tume ya huduma za umma nchini PSC imewaalika wakenya kutuma maombi ya nafasi ya Mkurugenzi wa mashtaka ya Umma nchini DPP.
Katika taarifa iliyochapishwa kutoka kwa PSC hii leo, yeyote aliye na nia ya kutwaa wadhifa huo lazima awe amehitimu na shahada ya sheria kutoka chuo kinachotambulika nchini na pia awe wakili katika mahakama kuu nchini pamoja na mahitaji mengine. MAELEZO ZAIDI
Wadhifa wa DPP uliachwa wazi baada ya Rais William Ruto kumteua Noordin Haji katika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS). Shughuli ya kutuma maombi ya kazi hii itaendelea hadi tarehe 12 mwezi ujao.
!!! Job Alert !!!
Call for Applications for the Position of Director of Public Prosecution (DPP). #IkoKaziKE pic.twitter.com/N7tRdSLZrZ
— Public Service Commission (PSC) (@PSCKenya) June 29, 2023