BY ISAYA BURUGU,30TH JUNE,2023-Rais William Ruto ametia Saini kuwa sheria mswada wa ugavi wa mapato kwenye kaunti wa mwaka 2023  na ule wa hazina ya usawazishaji vile vile wa mwaka 2023.

Miswada hiyo miwili sasa itawezesha kaunti zote 47 kupokea fedha katika mwaka mpaya wa matumizi ya kifedha unaoanza kesho Julai mosi.Sheria ya ugavi wa fedha katika kaunti  inazitengea serikali za kaunti shilingi bilioni 385.4  zitakazogawanywa kwa usawa.

Serikali  ya kaunti ya nairobi hata hivyo itapokea mgao mkubwa wa fedha hizo ikipokea shilingi bilioni.20.07.Sheria ya hazina ya usawa inaruhusu kutolewa kwa shilingi bilioni 10.3 za utoaji huduma muhimu kama vile maji,Barabara,umeme na afya  katika maeneo yaliyosalia nyuma kimaendeleo nchini.

Waliypkuwepo katika hafla ya kutia Saini miswada hiyo hivi leo katika ikulu ya Nairobi ni Pamoja na naibu rais Rigathi Gachagua, mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi, spika wa seneti  Amason Kingi, mkuu wa sheria  Justin Muturi na kiongozi wa wengi katika bunge la seneti  Aaron Cheruiyot, kati ya wengine.

June 30, 2023