BY ISAYA BURUGU 1ST JULY,2023-Watu kumi wamepata majeraha mabaya kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea eneo la kiokong Barabara kuu ya Bomet kuelekea Narok mwendo was aa kumi usiku wa kuamkia leo.

Majeruhi wamelazwa katika hospitali ya tenueki mjini Bomet wakiendelea kupokea matibabu.Naibu kamanda wa Bomet ya kati Bashir Ali amesema kuwa ajali hiyo imetokea baada ya gari dogo la kibinafsi kugongana ana kwa ana na matatu.

Ajali hiyo imetoa saa chache tu baada  ya ajali nyingine kutokea katika kaunti Jirani ya Kericho ambapo kufikia sasa waliofariki wamefikia 51.

 

 

July 1, 2023