BY ISAYA BURUGU 1ST JULY,2023-Washukiwa wanne wa wizi wa ng’ombe wamekamatwa alfajiri ya leo mjini Narok wakisafirisha ngombe  saba wanaokisiwa kuibwa kutoka eneo la Narok kusini.

Akithibitisha kisa hicho kamanda wa polisi Narok ya kati John Momanyi amesema polisi waliwapata wanne hao Ongari Togoyo, Elijah Naikumi ,Dickson Merku na driver wa Lori Samwuel Maingi wakiwa na Ngombe walioibwa Narok kusini.

Kwa  sasa wanazuiliwa  kaitiaka kituo cha polisi mjini Narok wakitarajiwa kufikishwa mahakamani pindi uchuguzi utakapokamilika.kamanda huyo wa polisi amesema serikali itawakabili vilivyo na mkono wa sheria wanne hao ili wawe  funzo kwa wanaotekeleza wizi

.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

July 1, 2023