BY ISAYA BURUGU 5TH JULY,2023-Mahakama kuu eneo la Kilgories Trasmara magharibi imechoma  zaidi ya gramu 390 ya bangi yenye thamana ya shilingi milioni 3.9 .

Akithibitisha kisa hicho msimamizi wa mahakama hiyo Paul Ochieng amesema tayari mshukiwa mkuu ametiwa mbaroni na amehukumiwa  miaka kumi na kutozwa faini ya milioni 1 ama ahudumie mwaka moja zaidi gerezani.

Msimamizi huyo amewataka wananchi kufanya biashara halali bila kuhusika na biashara iliyoharamishwa  humu nchini.

Ochieng amewataka wananchi kushirikiana na polisi  kuripoti visa vya ulanguzi  wa dawa za kulevya.

 

 

 

July 5, 2023