Tume ya kuwaajiri Walimu nchini TSC imetangaza nafasi za kazi 18,000 kwa tarajali yaani interns katika Shule za Sekondari msingi na nyingine 2,000 katika Shule za Msingi za Umma ili kusaidia utekelezaji wa Mtaala wa CBC.

Katika waraka, tume hiyo inasema walimu hao watapokea malipo ya kila mwezi ya Sh15,000, huku wale waliojiunga na JSS wakipata malipo ya kila mwezi ya Sh20,000.

Aidha, baada ya kukamilika kwa programu ya mafunzo ya kazi, walimu waliohitimu watapewa cheti. Ili kuhitimu kuwa mwalimu wa JSS, mwombaji lazima awe raia wa Kenya na mwalimu aliyesajiliwa na TSC.

Watu wenye ulemavu (PWDs) na walimu kutoka taasisi za TVET pia wamehimizwa kutuma maombi.Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni tarehe 10 Julai 2023.

July 5, 2023