Idara ya DCI imeomba muda wa siku 14 zaidi ili kuandaa kesi dhidi ya washukiwa wawili wa kampuni ya Brown Cheese, wanaodaiwa kuwadhulumu wafanyakazi wa kike katika kampuni hizo, kwa kuwalazimisha kuvua nguo ili kuchunguzwa iwapo wako katika kipindi cha Hedhi.

Wawili hao Rose Lydah Achieng Opondo na Vivian Oka Mukoko walifikishwa katika mahakama ya Limuru asubuhi ya leo ili kujibu mashtaka dhidi yao, ila sasa DCI imeomba muda zaidi wa kufanya uchunguzi na kuwasilisha kesi hiyo, kutokana na wingi wa mashahidi walio katika kesi yenyewe.

DCI aidha imeieleza mahakama kwamba wawili hao huenda wakasafiri nje ya nchini, hasa baada yao kusimamishwa kazini, au huenda wakahitiafiana na mashahidi.

 

July 7, 2023