Ruto Congo

Serikali za Kenya na Congo zimefikia makubaliano ya kuondoa hitaji la visa ili kurahisisha usafiri kati ya mataifa hayo mawili.

Muafaka huu ulitangazwa na Kiongozi wa Taifa, Rais William Ruto, ambaye yuko ziarani katika taifa la Jamhuri ya Congo, baada ya kikao cha pamoja na Rais Denis Sassou-N’Guesso wa Jamhuri ya Congo.

Rais Ruto alitoa taarifa ya pamoja na mwenyeji wake na kuelezea kuwa kuondolewa kwa vikwazo vya usafiri kutaimarisha biashara kati ya Kenya na Congo, huku akisisitiza kuwa Kenya ina lengo la kurejesha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Nairobi hadi mji wa Brazzaville.

Makubaliano haya ya kuondoa hitaji la visa yanaashiria hatua kubwa katika kukuza uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya Kenya na Congo. Hatua hii itachochea biashara na uwekezaji kati ya nchi hizi mbili, na kuwezesha raia wa mataifa haya kufanya safari za kitalii, kibiashara, na za kidiplomasia bila vikwazo vya visa.

https://twitter.com/WilliamsRuto/status/1677662210175139848?s=20

July 8, 2023