BY ISAYA BURUGU 10TH JULY 2023-Kinara wa upinzani Raila Odinga hivi leo ameabiri gari la uchukuzi wa umma kutoka nyumbani kwake mtaani Karen hadi kazini jijini Nairobi.

Raila ameungana na viongozi wengine katika safari yake hiyo ambapo ameabiri gari la umma kutoka nyumbani kwake Karen.

Ni hali ya utekelezaji wa semi za mkutano wa hadhara wa hivi maajuzi katika uwanja wa Kamkunji ambapo aliwaagiza wafuasi wake kuachana na magari ya kibinafsi na kutimia magari ya uchukuzi wa umma ili kutochangia katika utozaji wa ushuru wa juu uliyopendekezwa na serikali.

Kinara huyo wa Azimio la umoja amepanga mandamano mengine jumatano juma hili.

 

 

 

July 10, 2023