BY ISAYA BURUGU 12TH JULY 2023-Kenya na  Iran zimetia Saini aina tano za makubaliano ya kufanya kazi Pamoja katika Nyanja mbali mbali.Makubaliano hayo ni kuhusu Habari na mawasiliano,teknologia,uvuvi,uzalishaji mifugo,saw ana uwekezaji  kama nia moja ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

Hafla ya kutia Saini makubaliano hayo imeshuhudiwa na rais .William Ruto na mwenzake wa  Iran, Ebrahim Raisi, aliye kwenye ziara ramsi ya serikali humu nchini.

Rais Ruto amesisitiza umuhimu wa Iran kama mshirika  wa kimkakati wa Kenya.Wakati wa mkutano huo uliyoandaliwa katika ikulu ya Nairobi,rais Ruto na rais  Raisi wamejadiliana  kuhusu ushirikiano wakihistoria na kutambua sehemu za ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Viongozi hao pia wamefanya mazungumzo kuhusu njia za kuimarisha usawa wa utendaji baishara na kutumia fursa zinazojitokeza  kati ya mataiafa hayo

.Rais amesema uhusiano dhabiti na Iranni muhimu katika utekelezaji wa ruwaza yake ya bottom Up haswa kwenye Nyanja ya kilimo.

Rais wa Iran, Ebrahim Raisi, ameanza ziara ya kihistoria barani Afrika, akianzia na Kenya, ambapo amepata mapokezi makubwa ya saluti 21 na gwaride la kijeshi katika Ziara yake ya Kiserikali.

Kuwasili kwa Rais Raisi humu nchini  kunaashiria kuanza kwa ziara yake muhimu ya mataifa matatu barani Afrika, na ziara zilizofuata zimepangwa nchini Uganda na Zimbabwe.

Ziara hii ina umuhimu mkubwa kwani ni mara ya kwanza katika kipindi cha muongo mmoja kwa kiongozi wa Iran kuzuru bara hilo.

 

 

 

 

 

 

July 12, 2023