Kinara wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga amesitisha mkutano wa kupinga serikali uliokuwa umepangwa kufanyika katika uwanja wa Kamukunji.

Akihutubia wanahabari, Odinga alisema hatua hiyo ilichochewa na hatari kubwa ya ukosefu wa usalama inayotokana na machafuko yanayoshuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya taifa, akiongeza kuwa hatataka kuzidisha hali hiyo.

Alidai kuwa timu ya waandamanaji waliolipwa walivamia uwanja huo na kuharibu vifaa vilivyotumiwa kuinua jukwaa na pia kuwatawanya Wakenya waliokuwa na amani.

Odinga aliendelea kudai kuwa hawatalegea katika vita vyao dhidi ya serikali, huku akitoa wito kwa Rais William Ruto kusikiliza matakwa yao ili maandamano hayo yasije yakaendelea.

July 12, 2023