BY ISAYA BURUGU 13TH JULY 2023-Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki amewataka maafisa wa polisi kutowadhulumu wananchi kivyovyote wanapotekeleza majukumu yao.

Akizungumza alipongoza ufunguzi wa kituo cha polisi na afisi ya chifu huko Kiseriani kaunti ya Kajiado,Waziri amewataka polisi kujizatiti na kuendelea kuboresha uhusiano wao na wananchi ili waweze kufanikiwa katika mstakabali wao kazini.

Waziri amesema nykati za wananchi kuona afisa wa polisi kama adui zilipita na sasa ni wakati wa polisi na wananchi kushirikiana.

Aidha akirejelea visa vya mashambulizi ya kigaidi  ambavyo vimekuwa vikiripotiwa siku za hivi karibuni katika sehemu mbali mbali nchini,Waziri amesema serikali iki macho na itazidi kukabiliana na magaidi hao bila hofu wala kutishwa.Waziri pia amepongeza maafisa wa polisi waliojitolea kuweka Maisha yao hatarini ili kulinda mipaka ya kenya.

 

 

 

 

July 13, 2023