Waziri wa usalama wa ndani Kithure kindiki hii leo amefanya mkutano wa faraga na viongozi wa kaunti ya Narok ili kutathmni hali ilivyo katika mpaka Nkararu na Enooretet eneobunge la Trasmara magharibi.

Kufikia sasa watu 47 wametiwa mbaroni kuhusiana na machafuko ambayo yamekuwa yakishuhudiwa kati ya jamii za Isiria na Irwa-singishu.

Kindiki akiwahutubia wananchi katika mkutano huo ameonya kuwa serikali itawachukulia hatua kali za kisheria wale ambao wanaendelea kuchochea mzozo baina ya jamii hizo huku akiwaagiza wakaazi wa eneo hilo kusalimisha silaha zao kwa maafisa wa usalama.

Mkutano huo ulioandaliwa katika seminari ya mtakatifu Yosefu mjini Kilgoris pia ulihudhuriwa na mbunge wa eneo la Transmara magharibi Julius Sunkuli, mbunge wa Emurua Dikirr Johana Ngeno na mbunge mwakilishi wa kike katika kaunti ya Narok mama Rebecca Tonkei pamoja na maafisa wengine wa idara za usalama katika kaunti hii.

July 14, 2023