Kinara wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga sasa ameishutumu serikali kwa kutoa kile anachodai kuwa kikosi cha wauaji haramu.

Odinga, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari siku ya Jumamosi, alidai kuwa utawala wa sasa unatumia kitengo cha Operation Support Unit (OSU) kuwadhalilisha viongozi wa Azimio na wafuasi wao.

Kinara huyo amekilaumu kitengo hicho kwa vifo vilivyoshuhudiwa katika maandamano ya Jumatano huko Mlolongo, Kamkunji na Jogoo Road huku akishikilia kwamba alisema hatolegeza kamba katika vita vyake vya ukombozi wa nchi.

Wakati huo huo aliwaomboleza waliouawa na kukamatwa wakati wa maandamano hayo.

July 15, 2023