BY ISAYA BURUGU,29TH AUG 2023-Chama cha wanasheria nchini LSK na masharika ya haki za kibinadamu kimekashfu matamshi yar ais Wiliam Ruto kuwaonya wale waliowasilisha kesi mahakamani kuhusu umiliki wa kampuni ya sukari ya Mumias kuwa wanakumbwa na uwezekano wa kufurushwa humu nchini,kufungwa au kile rais alielezea kama safari ya Kwenda mbiguni matamshi wanayosema ni vitisho vya kifo.

Mwenyekiti wa LSK Eric Theuri anasema kuwa matamshi hayo ya rais yanaashiria kuwa anaweza kuipuuza katiba.LSK ambayo imehuzisha kitendo cha kutekwa nyara kwa mfanyibaishara Jaswant Rai kwa maswala yanayozungukza kiwanda cha sukari cha mumias,anasema mawakili watafuata kundi la watu watakaotishwa kwa kuwakilisha wateja waliowasilishwa kesi husika mahakamani.Sasa wanamtaka rais Ruto kuondoa matamshi hayo.

 Kwingineko Wabunge wanaoegemea upande wa  kinara wa upinzani Raila Odinga sasa wanamtaka Rais William Ruto kuiomba nchi msamaha hadharani kwa madai ya kutishia wawekezaji.Katika mkutano na waandishi wa habari bungeni, wabunge hao walimshambulia rais kwa kile walichokiita kutishia wawekezaji.Walikuwa kiongozi wa wengi katika seneti Stewart Madzayo, naibu wake Enoch Wambua na Seneta wa Migori Eddy Oketch.

Akizungumza eneo la Magharibi mwa nchi siku ya Jumapili, rais Ruto alizungumza kwa ukali kuhusu makampuni yanayokatisha tamaa mageuzi katika sekta ya sukari nchini.Rais aliwataka wawekezeji wote wa sukari wafuate sheria ama waondoke Kenya, waende jela au waende mbinguni.Lakini Madzayo alisema madai ya vitisho vya Rais ni tishio la moja kwa moja kwa maisha, kitu alichokitaja kuwa ni kinyume cha katiba .

 

 

August 29, 2023