EL Nino

Idara ya Utabiri wa Hali ya Anga nchini imeonya kuwa Taifa linakaribia kushuhudia mvua kubwa aina ya El Nino katika kipindi cha mvua za vuli, kuanzia mwezi wa Septemba hadi mwezi Oktoba mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na idara hiyo leo imeonyesha kuwa mvua hizo zinatarajiwa kuyakumba maeneo kadhaa nchini, yakiwemo maeneo ya Ziwa Victoria, kaunti za Kisii, Elgeyo Marakwet, Bungoma, Trans Nzoia, Pokot Magharibi, Vihiga, Laikipia, Nakuru na Narok.

Idara hiyo imeeleza kwamba kuna uwezekano wa asilimia 99 wa kushuhudia mvua hizi ambazo husababisha mafuriko katika maeneo mengi ya taifa, huku maeneo kama vile Gilgil, Narok mjini na eneo la Suswa yakitajwa kama yaliyo katika hatari kubwa ya kushuhudia mafuriko. Kipindi cha mvua kinatarajiwa kuendelea hadi mwezi Januari mwaka Kesho, huku mvua za kiwango cha juu zaidi kikitarajiwa mwezi Oktoba.

Dr. David Gikungu, ametoa ushauri kwa wakulima kutumia wakati huu vizuri na kuchukua tahadhari. Pia, wakazi wa maeneo ya nyanda za chini wanapaswa kuwa macho na kuchukua hatua za kujikinga. Idara ya Utabiri wa Hali ya Anga aidha imeahidi kuendelea kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusu hali ya anga.

https://twitter.com/MeteoKenya/status/1696566058042224807?s=20

August 30, 2023