Sukari

 

Gavana wa Kakamega Fernandes Barasa akitoa taarifa kuhusu matayarisho ya kuandaa kongamano la washikadau katika sekta ya Sukari. – Video | H.E FCPA Fernandes Barasa, OGW, Twitter

Magavana 14 kutoka kaunti za eneo la kiuchumi katika za ukanda wa ziwa, watakuwa sehemu ya kongamano la washikadau katika sekta ya sukari, lililoratibiwa kuandaliwa Mjini Kakamega. Kongamano hili limepangwa kufanyika katika bewa kuu la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro siku ya Ijumaa na Jumamosi.

Gavana wa Kakamega, Fernandes Barasa, ameonesha matumaini yake kwamba kongamano hili litakuwa na manufaa na pia umuhimu katika kufufua sekta ya ukulima wa miwa, hasa katika eneo la Magharibi ambalo limekuwa likikumbwa na changamoto nyingi katika viwanda vya sukari. Kongamano hili linatarajiwa kutoa suluhisho la kina kuhusu jinsi ya kurejesha ufanisi katika viwanda vya sukari, pamoja na njia za kusaidia wakulima na maeneo yanayojihusisha na kilimo cha miwa kunufaika na sekta hii muhimu.

Pamoja na magavana, viongozi wa serikali kuu wakiwemo wale wa wizara ya kilimo, viwanda na hata vigogo wa kisiasa kutoka ukanda wa Magharibi watakuwa sehemu ya kongamano hilo. Kongamano hili ni hatua muhimu kuelekea kuimarisha uzalishaji wa sukari na kutoa fursa za kiuchumi katika eneo hilo la kiuchumi katika ukanda wa ziwa

 

September 7, 2023