Serikali ya Kaunti ya Narok kupitia afisi ya kilimo na mifugo imeonya wafugaji eneo la Narok Magharibi hasa Endonyorasha kusitisha usafirishaji mifugo ili kutoa nafasi kwa maafisa wa afya kutoa chanjo dhidi ya mkurupuko wa ugonjwa wa kimeta yaani Anthrax.

Akiongea na wanahabari afisini mwake, Joyce Keshe ,waziri wa Kilimo na mifugo aliyeomboleza na waathiriwa alisisitiza kuwa usafiri wa mifugo utakubalika pindi tu chanjo kwa mifugo yote kijiji cha Endonyo-rasha wadi ya siana na viungani mwake itakapomalizika ili kuzuia maafa zaidi.

Keshe akihakikishia uma kuwa mashirika husika yamejiunga kufuatia amri ya Gavana Patrick Ole Ntutu hususan kudhibiti msambao Zaidi kwa maeneo mengine huku takriban chanjo elfu sabini zikiwa tayari kwa mpango huo.

Aliongeza kuwa hamasa inaendelea kwa wanavijiji kusitisha ulaji wanyama ambao kiini cha kifo hakiulikani.Daktari Gideon Kesha ambaye ni Mkurugenzi wa mifugo Kaunti ya Narok anatoa taswira kuhusu kimeta akieleza kuwa ni aina ya bakteria iliyo na uwezo wa kustahimili mazingira na hupatikana kwa wanyama pori ambao wakifa kuathiri mazingira ya binadamu.

Kesha anahoji kuwa hali hii huathiri wanyama kama ng’ombe lakini ushirikiano na asasi husika imesaidia kudhibiti maambukizi huku akieleza dalili za ugonjwa huu ambao wafugaji na wakulima huelezwa.

Anajuta kuwa baadhi ya wakaaji wamepuzilia mbali nyama mbovu na kula swala ambalo limesalia hatari kwa afya akieleza aina za dalili ya maambukizi kwa binadamu na jinsi ya kudhibiti mnyama aliyeaga.

Kesha anazidi kueleza kuwa ni bora kuchanja wanyama pori lakini ni gharama kubwa kwa serikali ila idara ya kulinda wanyama pori ya KWS wamesalia macho kupasha ujumbe iwapo hatari ya msambao wa kimete upo na kuchukua hatua mwafaka.

Anatoa mawaidha kuwa shilingi 1500 inatosha kuchanja ngombe 50 na ni vyema kwa mfugaji kuchanja wanyama wake ili kudhibiti msambao kabla ya hasara kubwa. Anazidi kukumbusha kuwa maafisa wa afya wako gangari katika vichinjio rasmi vyote na iwapo mnyama atapatikana kuwa ameambukizwa kimeto au ungonjwa hatari hatu za tahadhari zitachukuliwa kabla na baada ya kuchinjwa.

Haya yanajiri siku moja baada ya waziri wa afya na usafi Antony Namunkuk wa Kaunti kuzamia swala hili kama la dharura akiwarai wakaazi maeneo yaliyoathirika kuwasili haraka kwa vituo vya afya iwapo wanahisi dalili mbaya za afya ili kutibiwa.

Miezi miwili iliyopita watalii walifurika mbuga ya hifadhi ya kitaifa ya Maasai Mara ambako takriban nyumbu na pundamilioa milioni tatu walivuka mto mara kutoka mbuga ya Serengeti nchini Tanzani hii ikiwa kivutio cha maajabu ya nane ulimwenguni ambapo pia wao hujumuika na wanyama wa kawaida hivyo kusambaza magonjwa kadhaa.

September 21, 2023