BY ISAYA BURUGU 23RD OCT 2023-Mahakama ya Nairobi imemwachilia anayedaiwa kuwa wakili ghushi Brian Mwenda kwa dhamana ya Ksh.200,000 pesa taslimu.Hakimu Mkuu wa Milimani, Lukas Onyina, amesema upande wa mashtaka haukutoa sababu za msingi za kumnyima dhamana mshtakiwa.

Mwenda wiki iliyopita alifikishwa mahakamani  na kusomewa mashtaka sita ya kutoa hati ya uongo, kutengeneza hati ya uongo pamoja na cheti cha kufanya kazi.Alikanusha mashtaka yote mbele ya Hakimu Mkuu wa Nairobi Lukas Onyina.

Njagi alikamatwa na maafisa wa upelelezi wa DCI mnamo Oktoba 18 baada ya kufichuliwa kuwa wakili bandia.Kesi hiyo itatajwa Novemba 7.

Upande wa mashtaka uliiomba mahakama kumnyima dhamana Mwenda kwa madai kuwa iwapo ataachiliwa hatahudhuria kesi mahakamani.

Mahakama pia iliambiwa kwamba mwenendo wa Mwenda unaonyesha kwamba hajali sheria, na kwamba alikwepa polisi kwa zaidi ya siku nne.

 

 

 

 

 

JUMA LA SHERIA

October 23, 2023