Photo of SGR Train in Kenya

BY ISAYA BURUGU,1ST NOV,2023-Kampuni ya Kenya Railways imeongeza nauli katika  maeneo yote inayopeana huduma zake za safari  kwa asilimia 50.

Katika arifa  ya hivi punde, abiria wa Mombasa sasa watalipa Sh1,500 kuanzia Januari 1, 2024, kutoka Sh1,000 ya sasa.

Tikiti zilizonunuliwa kabla ya wakati huo, hata hivyo, hazitaathirika.Kwa wale wanaotaka kusafiri na daraja la kwanza, watalazimika kulipa Sh4,500, kutoka Sh3,000.Nauli kutoka Kibwezi hadi Mombasa itagharimu Sh890 huku Voi hadi Mombasa ikigharimu Sh440.

Bei hizo ziliorodheshwa upya kwa Huduma ya abiria wa Madaraka Express, Huduma ya Reli ya Nairobi Commuter, Treni ya Safari ya Kisumu na Treni ya Safari ya Nanyuki.

 

 

November 1, 2023