Serikali ya Kitaifa imezindua rasmi mitambo ya kidijitali inayolenga kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika Chuo cha Serikali eneo la Kabete, jijini Nairobi, ukiongozwa na Katibu wa Wizara ya Usalama wa Ndani, Bwana Raymond Omollo.

Mitambo hii ya kidijitali kwa jina la Beta, inalenga kuboresha ufanisi na uwazi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikilenga kuzuia kukwama kwa miradi hiyo kutokana na ukosefu wa ufuatiliaji wa karibu. Omollo ameelezea kuwa mitambo hiyo itachangia sana katika kuimarisha utendakazi wa serikali na kuhakikisha kuwa miradi yote inayotekelezwa inafuatiwa kwa karibu.

Makamishna wa serikali
Kamishna wa Kaunti ya Narok Isaac Masinde (Wa Pili Kushoto) akiwa na maafisa wengine kwenye hafla ya uzinduzi wa Mitambo ya Beta katika chuo cha serikali | Picha: Raymond Omollo (Mtandao wa X)

Waratibu wa Mikoa, Makamishna na manaibu wao kutoka pembe tofauti za taifa wametajwa kuwa sehemu muhimu ya zoezi hilo, kwani wanatarajiwa kusaidia katika kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo na kutoa taarifa kwenye mitambo hiyo ya kidijitali.

SOMA PIA: Makamishena 20 wahamishwa, 15 wasalia huku manaibu kamishena 12 wakipandishwa ngazi.
November 22, 2023