Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki ameagiza kuchunguzwa, kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa watu katika Kaunti ya Lamu wanaotumia mitandao ya kijamii kuchochea chuki za kikabila na kidini.
Haya yanajiri kufuatia video iliyosambaa kwa baadhi ya viongozi wakidai kuunda baraza la mawaziri ili kuzitimua baadhi ya jamii kutoka kaunti ya Lamu.
Akizungumza baada ya kutathmini hali ya usalama katika maeneo ya Salama na Poromoko huko Lamu Magharibi, Prof Kindiki alitoa onyo kwa wale wanaotumia mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari kueneza chuki na vurugu kwa misingi ya kidini, kikabila na kisiasa.
Alisema serikali imesalia na azma ya kutokomeza vitisho vinavyotolewa na magaidi, itikadi kali na wahalifu wengine katika kaunti hiyo. Kindiki alibainisha kuwa baada ya kukagua mazingira ya utendakazi yaliyopo, vituo vya ziada vya ulinzi vimeanzishwa ili kuimarisha usalama katika maeneo ya Marafa, Widho, Juhudi, Salama na maeneo jirani.
The Government remains seized of the security situation in Lamu County to neutralize the threats posed by terrorists, extremist ideologies and other criminals.
It is gratifying to note the significant progress made by the Multi-Agency Operation Linda Boni, and the commendable… pic.twitter.com/AzGLdRHr6q
— Kithure Kindiki (@KindikiKithure) December 7, 2023