Ajali Nakuru

Watu 15 wamepoteza maisha yao katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika eno la Twin Bridge, kwenye barabara kuu ya Nakuru – Eldoret. Ajali hiyo ilihusisha basi moja la kampuni ya Classic Kings of Congo na matatu ya Kampuni ya Northways Shuttle, ambazo ziligongana ana kwa ana mwendo wa saa tisa kasorobo asubuhi.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Kuresoi Kaskazini, amethibitisha ajali hiyo akieleza kwamba waliofariki ni watu 8 wazima na watoto 7 walio kati ya umri wa mwaka mmoja na miaka 15. Manusura na waliojeruhiwa walipelekwa kwenye hospitali ya Kaunti ya Molo kwa matibabu. Kamanda huyo ameeleza kwamba basi hiyo ilipoteza mwelekeo katika eneo hilo lenye mteremko, ka kugongana ana kwa ana na matatu hiyo.

SOMA PIA: Watu 2 Waangamia Katika Ajali Mbili Tofauti za Barabarani Kaunti ya Narok.

Wito unaendelea kutolewa kwa madereva kuwa waangalifu na makini zaidi barabarani ili kuepuka ajali za aina hii. Wananchi wa eneo hilo aidha wanaiomba serikali kuboresha barabara hiyo kwa kuipanua na kuweka kuta za barabarani ili kuzuia ajali kama hizi kutokea tena.

 

January 9, 2024