Naibu rais Rigathi Gachagua ameendelea kukashifu vita vya kisiasa vinayoshuhudiwa katika eneo la mlima Kenya akisema kuwa vita hivyo ni vya kutawanya eneo hilo badala ya kujenga.

Akizungumza katika kaunti ya Nayndarua, Gachagua amewataka viongozi wanaoendeleza siasa hizo kuwatumikia wananchi ikizingatiwa kwamba bado ni mapema kuzungumzia uchaguzi wa mwaka 2027.

Kuhusu suala la uraibu wa pombe haramu katika eneo la mlima Kenya, Rigathi amesema kuwa ni lazima serikali ishinde vita dhidi ya pombe haramu, dawa za kulevya, na matumizi mabaya ya dawa ili kuokoa kizazi chetu. Na ili vita hivyo vifanikiwe na kuwa endelevu, lazima kuwe na mifumo sahihi ya kisheria.

January 23, 2024