Taasisi ya utafiti TIFA hii leo imetoa ripoti ya utafiti kuhusu utendakazi na safari za nje ya nchi za mawaziri nchini. Kwenye ripoti hiyo, waziri wa Utalii na Alfred Mutua ameorodheshwa kama Waziri aliyesafiri zaidi katika mataifa ya kigeni lakini hafanyi kazi sana humu nchini.

Safari za kimataifa za bw. Mutua zinafikia asilimia 28% na shughuli zake za ndani ziko asilimia 72% ambapo safari 23 zilizorekodiwa katika kaunti 6 pekee.

Mutua anafuatwa kwa karibu na Waziri wa Utumishi wa Umma Moses Kuria ambaye safari zake za kimataifa zilifikia asilimia 16%, Waziri wa Madini Salim Mvurya asilimia 14%, Njuguna Ndung’u wa Hazina ya kitaifa ana asilimia 13% huku mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi akiwa na 12%.

Ripoti hiyo aidha imemorodhesha Waziri wa usalama wa Ndani Kithure Kindiki kama Waziri anayefanya kazi zaidi nchini baada ya kufanya shughuli 192 za ndani zilizorekodiwa.

Kindiki, ambaye hajafanya safari za nje, amezuru kaunti nyingi zaidi kwani amefanya safari katika kaunti 41 kati ya 47 zote.

February 7, 2024