Waziri wa Afya Susan Nakuhmicha amesisitiza haja ya kuchukuliwa hatua kuhusu usalama wa chakula wakati wa hotuba yake katika kikao cha 54 cha Kamati ya Codex kuhusu Usafi wa Chakula.
Waziri huyo aliangazia athari za kutisha za magonjwa yanayotokana na chakula duniani, huku zaidi ya watu nusu bilioni wakiugua kila mwaka na vifo nusu milioni vikirekodiwa, hasa Afrika.
Nakhumicha aidha alieleza kujitolea kwa muda mrefu kwa Kenya kuunga mkono juhudi za kimataifa katika viwango vya usalama wa chakula kama mwanachama wa Tume ya Codex tangu 1969.
Alitoa shukrani kwa Marekani kwa kuandaa kikao hicho na Serikali ya Kenya na kuwataka washikadau wote kutanguliza usalama wa chakula na viwango vya usafi, akisisitiza jukumu lao kuu katika ajenda za afya ya umma.