Jenerali Charles Muriu Kahariri ameapishwa na kusimikwa rasmi kama mkuu wa majeshi nchini Kenya asubuhi ya leo, baada ya uteuzi wake siku ya Alhamisi.
Hafla hiyo muhimu ilifanyika katika Ikulu ya Nairobi, ambapo Kiongozi wa Taifa, Rais William Ruto, alimsimika Jenerali Kahariri na kumfanya afisa wa nyota nne, na sasa ataongoza idara ya ulinzi ya Kenya kama mkuu wa majeshi.
Jenerali Kahariri awali alikuwa naibu wa mkuu wa majeshi wakati wa uongozi wa aliyekuwa mkuu wa majeshi, marehemu Jenerali Francis Ogolla, aliyefariki katika ajali ya helikopta mwezi jana. Katika majukumu yake mapya, Jenerali Kahariri atasaidiwa na Luteni Jenerali John Omenda, ambaye naye aliteuliwa kushikilia wadhifa huo siku ya jana.
H.E Hon Dr William Samoei Ruto, C.G.H, President of the Republic of Kenya and Commander-in-Chief of the Defence Forces, pursuant to section 9 (2) (a) of the KDF Act, has promoted Lt Gen Charles Muriu Kahariri to the rank of General & appointed him The CDF.https://t.co/uwYBUqeqVB pic.twitter.com/FClNACBaq4
— Kenya Defence Forces (@kdfinfo) May 2, 2024
Pamoja na uteuzi wa Generali Kahariri, kulikuwa na uteuzi na kupandishwa vyeo vingine muhimu. Maj-Jen Fatuma Gaiti Ahmed aliteuliwa kuwa kamanda mpya wa Jeshi la Anga la Kenya, huku Maj-Jen Paul Owuor Otieno akipandishwa cheo kuwa kamanda mpya wa wanajeshi wa Jeshi la Wanamaji. Wote hawa pia wameapishwa hii leo.