Waziri wa hazina ya kitaifa John Mbadi amekabidhiwa rasmi ala za ofisi hiyo na mtangulizi wake Njuguna Ndung’u, ambaye anaondoka wakati ambapo wakenya wanaendelea kulalamikia gharama ya juu ya maisha kufuatia ushuru wanaotozwa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wizara ya hazina ya kitaifa mapema leo, Mbadi alikiri kuwa kutakuwepo na changamoto ya kutekeleza miradi ya serikali bila ya mswada wa fedha wa mawaka 2024 ambao ulitupiliwa mbali kufuatia maandamano ya vijana yaliyotikisa nchi.

Aidha alieleza kuwa mswada huo hauezi kurejeshwa tena, ila watafuta mbinu za kutafuta fedha za ziada ambazo zitatumika kuendesha shuguli za serikali.

Kwa upande Bw. Ndung’u aliyekuwa waziri wa hazina ya Kitaifa alielezea hatua alizopiga na changamoto alizokumbana nazo alipokuwa ameshikilia wadhifa huo.

Wakati huo huo ambaye alichaguliwa kuwa waziri wa ulinzi baada ya kuhamishwa kutoka katika wizara hiyo ya mazingira.

Duale ambaye alikuwa Waziri wa ulinzi katika baraza lililovunjwa, alitoa onyo kwa wanyakuzi wa misitu ya umma huku akiahidi kuwa chini ya uongozi wake atahakikisha kuwa misitu yote iliyonyakuliwa inarejeshwa.

Hali kadhalika aliwahimiza wakenya kukumbatia upanzi wa miti ili kufikia lengo la kupanda miti bilioni 15 ifikapo mwaka 2032.

August 12, 2024