Amos Nyaribo

MCA katika Bunge la Kaunti ya Nyamira wamewasilisha mswada wa kumbandua Gavana Amos Nyaribo madarakani kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi na ukiukaji wa Katiba.

Mswada huo, uliowasilishwa na Mwakilishiwadi mteule wa chama cha Wiper Evans Juma Matunda, unalenga kumbandua Nyaribo ofisini, kwa kutofuata mwongozo wa utendakazi.

Mswada wa Kumbandua NyariboKikao cha kujadili mswada huo kimepangwa kufanyika Alhamisi, tarehe 12 Septemba, kuanzia saa tatu unusu asubuhi katika ukumbi wa Bunge la Kaunti ya Nyamira. Mswada huu unatarajiwa kuchochea mjadala mzito miongoni mwa wawakilishi na wadau wa kisiasa, huku wengi wakiangalia kwa karibu hatma ya uongozi wa gavana Nyaribo.

September 10, 2024