Gavana wa Kaunti ya Narok, Patrick Ntutu, anatarajiwa kuanza ziara ya siku nane katika eneo bunge la Emurua Dikirr leo, kwa lengo la kuzindua na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo. Ziara hiyo pia itatoa fursa kwa wananchi wa maeneo mbalimbali ya Emurua Dikirr kukutana na viongozi wa kaunti, ambapo watapata nafasi ya kujadili maendeleo na changamoto zinazowakabili.
ANNOUNCEMENT: EIGHT-DAY DEVELOPMENT TOUR OF EMURUA DIKIRR CONSTITUENCY
Starting tomorrow morning at 8:00 AM, I will embark on an eight-day tour across Emurua Dikirr Constituency to inspect and commission completed development projects. During this period, I will also hold public… pic.twitter.com/pxIzUzCvok
— Governor Patrick Ole Ntutu (@OleNtutuK) October 14, 2024
Juma lililopita, Gavana Ntutu alifanya ziara sawia katika eneo bunge la Narok Kaskazini, ambapo alizindua miradi kadhaa ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa soko jipya mjini Narok, soko la kisasa na mnada katika eneo la Rotian, kufungua barabara zilizokamilika pamoja na miradi mingine.
Miradi hiyo inalenga kuboresha maisha ya wakazi wa maeneo hayo na kuchangia katika ustawi wa kiuchumi wa kaunti nzima ya Narok.