Nyuki… wadudu wadogo, lakini wenye umuhimu mkubwa kwa maisha ya wanadamu. Wadudu ambao wanatambulika kwa bidii zao na uwezo wa kipekee wa kutengeneza asali na pia kusaidia mimea mbalimbali katika uzalishaji. Lakini je unafahamu kwamba ukulima wa nyuki au apiculture ni mojawapo ya biashara zenye faida zaidi kote duniani?