Serikali imetangaza kuwa zoezi la kitaifa la kuchanja mifugo kote nchini litazinduliwa wiki ijayo. Mkurugenzi wa huduma za mifugo Allan Azegele, amesema kuwa zoezi hilo litaanza mara moja baada ya kuzinduliwa kutokana na hatari zinazochangiwa na magonjwa ya mifugo.

Zoezi hilo litaanza katika Kaunti ya Laikipia na litatekelezwa katika ngazi ya kaunti.Wakurugenzi wa Kaunti wa Huduma za Mifugo watasimamia zoezi hilo.

Azegele ameongeza kuwa zoezi hilo limechochewa na magonjwa ya mifugo ambayo yanaendelea kukithiri.

Aidha zoezi hilo limekabiliwa na upinzani mkubwa haswa kutoka kwa jamii za wafugaji wakisema kuwa serikali haijatoa hamasisho ya kutosha kuhusu chanjo hiyo.

January 22, 2025

Leave a Comment