Leonard Mambo mbotela

Mtangazaji mkongwe wa redio, Leonard Mambo Mbotela, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 85. Familia yake imethibitisha kuwa Mbotela alifariki Ijumaa, Februari 7, baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Mbotela anafahamika zaidi kwa kipindi chake maarufu “Je, Huu Ni Ungwana?” kilichorushwa hewani kupitia Shirika la Utangazaji la Kenya (KBC) kwenye Redio ya Taifa na televisheni. Alistaafu kutoka KBC mnamo 2022, baada ya kutumikia tasnia ya utangazaji kwa miongo kadhaa.

Alizaliwa mwaka 1940 huko Mombasa na alianza safari yake ya utangazaji mwaka 1964, alipojiunga na Sauti ya Kenya (VoK), ambayo baadaye ilibadilishwa jina kuwa KBC.

Mbali na taaluma yake ya utangazaji, Mbotela anakumbukwa kwa tukio la Agosti 1, 1982, ambapo alilazimishwa kwa mtutu wa bunduki kutangaza kupitia redio kwamba serikali ya Rais wa zamani Daniel arap Moi ilikuwa imepinduliwa wakati wa jaribio la mapinduzi lililoshindikana.

February 7, 2025

Leave a Comment