Kampeni ya msimu wa kwaresma wa mwaka 2025 ulizindualiwa hii leo katika jimbo kuu katoliki la Mombasa. Kauli mbiu kwenye kampeni hii ambayo itaanza na kipindi cha kwaresma siku ya Jumatano ya majivu ni Kenya Tunayoitamani.
Askofu Peter Kamomoe ambaye anasimamia tume ya haki na Amani katika baraza la maaskofu wa kanisa katoliki KCCB, aliwahimiza wakristu kuainisha matamanio yao na kauli mbiu ya mwaka huu kama njia mojawapo ya kuimarisha haki katika jamii na taifa la Kenya.
Kando na uzinduzi wa kampeni hii, maaskofu katika hotuba yao ya pamoja, wameitaka serikali kutatua mzozo uliopo kwenye sekta ya afya haswa bima ya afya ya jamii SHA ambayo imeshuhudia wagonjwa wengi wakikosa kupokea huduma za matibabu kufuatia changamoto zilizopo kwenye bima hiyo.
Vilevile wameitaka serikali kusitisha siasa za ubabe na kuangazia masuala ya maendeleo yatakayoimarisha maisha ya wakenya na kuinua uchumi wa taifa.